Vincent Kompany anaondoka Man City kwenda kuwa kocha mchezaji

Nahodha wa Man City ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany ametangaza kuwa anaondola Man City na kuamua kurejea nyumbani kwao Ubelgiji, ambapo ndiko alikozaliwa na kukulia. Kompany anaondoka Man City baada ya kudumu kwa miaka 11 ila ameamua kurudi nyumbani kwao wakati huu akiwa na umri wa miaka 33, hivyo anarudi katika club yake iliyomlea ya Anderlecht akiwa na jukumu la kwenda kuwa kocha mchezaji. Nahodha wa Man City ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany ametangaza kuwa anaondola Man City na kuamua kurejea nyumbani kwao Ubelgiji, ambapo ndiko alikozaliwa na kukulia.

Kompany anaondoka Man City baada ya kudumu kwa miaka 11 ila ameamua kurudi nyumbani kwao wakati huu akiwa na umri wa miaka 33, hivyo anarudi katika club yake iliyomlea ya Anderlecht akiwa na jukumu la kwenda kuwa kocha mchezaji.

Kwa taarifa hizo ni wazi Kompany anaenda kuandaliwa kuwa kocha wa club ya Anderlecht,  Kompany anaondoka Man City akiwa kaichezea jumla ya michezo 360, akifunga magoli 20, mataji 4 ya EPL, League Cup 4, FA Cup 2 na Ngao ya Jamii 2. Kompany alianzia soka lake katika Academy ya Anderlecht akiwa na umri wa miaka 14 2000 na 2003 akapandishwa timu ya wakubwa ya Anderlecht na kucheza kwa misimu mitatu, 2006 akajiunga na club ya Humberger SV aliyodumu nayo kwa misimu miwili na kwenda Man City 2008.

Waziri Mwakyembe ampongeza Mbwana Samatta

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ametoa pongezi kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuibuka mabingwa wa Ubelgiji.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Samatta amefanya jambo kubwa kwa kuzingatia Ubelgiji ni moja ya mataifa makubwa tena yanayofanya vizuri kwenye mchezo wa soka duniani.

”Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo”, amesema.

Mbwana Samatta ambeye ni mchezaji wa zamani wa Simba, TP Mazembe na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016, mpaka sasa ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Ubelgiji akiwa amefunga magoli 20.

Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ambapo mwaka huo pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.