Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii wa Tanzania kuoa nje ya nchi
yao, hali inayopelekea watu wengi kujiuliza kuna shida gani kwa wanawake
wa Tanzania.
Wasanii kama Alikiba, Ben Pol na AY, wote wamefanikiwa kuoa nje ya nchi,
huku Ben Pol akiwa mbioni kumuoa mpenzi wake Anerlisa ambaye ni raia wa
Kenya baada ya kumvisha pete ya uchumba hivi karibuni. Alikiba pia
ameoa Kenya na AY amemuoa mrembo raia wa Rwanda.
Mwijaku ambaye ni muigizaji maarufu nchini na mtu maarufu katika
mitandao ya kijamii, amezitaja sababu 5 zinazopelekea wasanii wa
Tanzania kuamua kuoa nje ya nchi.
Sababu ya kwanza ameitaja kuwa ni uoga wa wasanii wa kiume maarufu
Tanzania, kutokana kuwa wanahisi wanawake wa Kitanzania wanawafahamu nje
ndani.
Sababu ya pili ni kuogopa kuchaguliwa au kukosolewa uchaguzi wa wanawake
wao na ndugu wa familia. Mtazame hapa chini Mwijaku akielezea zaidi
sababu hizo.
Category: udaku
”Nafuatwa na wanaume 500 kwa siku” – Miss Bella
KwaMsanii wa Bongo Fleva Isabela Mpanda ‘Miss Bella’ amesema kuwa hutongozwa na wanaume ambao idadi yao inaweza kufikia 500 kwa siku na haoni ajabu kwake kama mwanamke.
Bella amesema kuwa kufuatia hali hiyo ya kufuatwa sana limepelekea pia kuhongwa vitu vya gharama, lakini hategemei mali wala kitu chochote kutoka kwa mwanaume ili aendeshe maisha yake kama wanavyofanya baadhi ya mastaa wa kike badala yake anapambana kivyake kufikia malengo yake.

“Sishangai na sio ajabu mimi kuhongwa lakini sitegemei sana hivyo vitu vya kupewa mimi najipambania mwenyewe”, amesema Bella.
Bella amekuwa akiingia kwenye migogoro na baadhi ya watu kwenye mitandao, ambao wamekuwa wakidai kuwa anaigiza maisha ya kwenye mitandao na si maisha yake halisi.
The Journey Begins
Thanks for joining me!
Good company in a journey makes the way seem shorter. — Izaak Walton

