Mapacha Paul na Peter Okoye wa P-Square kuburuzana mahakamani kisa picha

Wasanii wakubwa nchini Nigeria, ambao pia ni mapacha Peter na Paul Okoye huenda wakaburuzana mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa Paul ametumia picha ya mwenzie kwenye tangazo la tamasha lake nchini Angola.

Peter ambaye yeye ndiye mlalamikaji, amesema kuwa anatarajia kwenda mahakamani kumshtaki ndugu yake, Paul Okoye, kwa kutumia picha zake kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo la muziki.

Kwahiyo wameamua kutumia picha yangu ili wauze tiketi za show yao huko Angola. Nyie mapromota na uongozi mzima mwanasheria wangu atalifuatilia suala hilo mapema iwezekanavyo,” ameandika Peter kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, tayari Paul Okoye ameshafanya show yake jana Jumapili Mei 26, 2019 usiku nchini Angola.

Peter na Paul ni mapacha na zamani waliunda kundi la P-Square ambalo lilipata umaarufu zaidi duniani kupitia nyimbo kadha wa kadha ikiwemo Personally, Temptation na nyinginezo.

Kwasasa kundi hilo limevunjika kwa sababu mbalimbali ikiwemo za maslahi binafasi na kifamilia, Ingawaje kumekuwa na masuluhisho kadhaa ya kurudisha kundi hilo.

Shamsa Ford ajitangaza kuwa single.

 Shamsa Ford na Mume wake ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini Chid Mapenzi penzi lao linasemekana  kuwa limevunjika, ingawa kwa upande wao hakuna aliyefunguka kuhusu hilo.

Tetesi hizo zimezidi kusambaa kwenye mtandao kijamii baada ya caption aliyoiandikaShamsa kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amejiita single mama na ndipo mashabiki walipopigia msitari na kusema kuwa ndoa kati ya Shamsa na Chid Mapenziimevunjika, ndoa hiyo ilifungwa September 2, 2016.

“Morning my people..kumekucha jamani ..wale masingle ladies kama mm jamani achieni mashuka mkatafute vijicent vya watoto wenu maana mjini pagumu bila kuchakarika na hizi shule za watoto wetu vingereza vingi mpaka mtu unaogopa kurudi nyumbani mapema unavizia mpaka mtoto awe amelala😀”

Sabuni Hizi Zinaongoza Kuachanisha Ndoa

Ukienda guest au hoteli yoyote hapa TZ unakuta sabuni hizi za EVA zimewekwa kwenye bafu la choo cha chumba ulichopanga..

Kwa kawaida ni adimu sana kuikuta inatumika nyumbani,hivo nadhani hata watengenezaji wa hizi sabuni wanajua kuwa soko lao kubwa ni nyumba za wageni..

SABUNI HIZI ZINA HARUFU SANA..
Wanawake wanazijua sana harufu za sabuni hizi na ikitokea umerud nyumbani na harufu yake una maswali magumu ya kujibu,.

Inavosemekana baadhi ya ndoa zimevunjika kwasababu ya harufu ya hizi sabuni..

Ni wakati mwafaka wa kampuni inayozitengeneza kuangalia kama kuna umuhimu wa kuweka harufu kali kwenye bidhaa yao hii..

Wasiozijua kwa jina picha hiyo hapo..