Zinedine Zidane amesema kuwa hatamtumia tena msimu ujao mshambuliaji wake, Gareth Bale .Zidane amesema kuwa kwenye mchezo huu wa mwisho asingeli muingiza Bale, hata kama wachezaji wote wa sub wangeisha.
“Sitamjumuisha (Bale) kwenye kikosi changu cha msimu ujao, kuhusu mchezo huu kumuaga kwa heshima sikufikiria. Nadhani hata wachezaji wa ziada wangeisha nisingeweza kumuingiza uwanjani,” amesema Zidane.Real Madrid wamemaliza msimu huu wakiwa nyuma ya alama 21 nyuma ya mabingwa wapya wa La Liga FC Barcelona.