De Oranje are ready to rise again.

Kila taifa lina muundo na utamaduni ambao unaleta ladha ya soka lake.:✍️Mwaka 1974 Uholanzi ilisheheni vipaji vikubwa sana. Licha ya kuwa na kizazi cha dhahabu wakashindwa kunyakua kombe la dunia. Kikosi kile kilitajwa kuwa kikosi bora sana katika historia ya soka.:✍️ 2010 walijitahidi kufikia kuweka historia ya kunyaku taji la lakini wakazidiwa na Wahispania. Uholanzi ile ilishehen kizazi cha dhahabu haswa. Akina Roben, Van De Sar, Welsej n.k.:✍️ Baada ya 2014, Uholanzi ikatoka kwenye Total Football na kwenda Total Failure. Pombe kali ikalevya kizazi cha waholanzi. Soka lao likawa butu.:✍️ Swahiba wangu mmoja anayeishi Uholanzi aliniambia akipokwenda Uholanzi mwaka 2012, asilimia kubwa ya waoto wa miaka 9+ utamkuta aidha anacheza vilabu vya mtaani au yupo kwenye akademi ya soka ya klabu kubwa.:✍️ Akaniambia miaka 8 ijayo uholanzi itaisha sana. Kila kijana hapa ana ndoto ya kuwa Cryjuff au Roben.:✍️ Mtaa kama Tandale unakuta una vilabu sio chini ya 7. Jambo la kuvutia utakuta Vipo vilabu vidogo kabisa vya watoto wa chini ya miaka 9.:✍️Madhara yake tumeona kizazi cha sasa vha Uholanzi. Tazama ile cream ya Ajax, angalia nyongo za Van Djik, Gigi zilivyochafukwa. Hata yule Depay aliyembwele OT nae amekuwa wa moto.:✍️ Ukitaka kuamini maneno yangu, leo watazame hawa vijana wakisakata kabumbu vs England:De Oranje are ready to rise again.

Leave a comment