Vincent Kompany anaondoka Man City kwenda kuwa kocha mchezaji

Nahodha wa Man City ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany ametangaza kuwa anaondola Man City na kuamua kurejea nyumbani kwao Ubelgiji, ambapo ndiko alikozaliwa na kukulia. Kompany anaondoka Man City baada ya kudumu kwa miaka 11 ila ameamua kurudi nyumbani kwao wakati huu akiwa na umri wa miaka 33, hivyo anarudi katika club yake iliyomlea ya Anderlecht akiwa na jukumu la kwenda kuwa kocha mchezaji. Nahodha wa Man City ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany ametangaza kuwa anaondola Man City na kuamua kurejea nyumbani kwao Ubelgiji, ambapo ndiko alikozaliwa na kukulia.

Kompany anaondoka Man City baada ya kudumu kwa miaka 11 ila ameamua kurudi nyumbani kwao wakati huu akiwa na umri wa miaka 33, hivyo anarudi katika club yake iliyomlea ya Anderlecht akiwa na jukumu la kwenda kuwa kocha mchezaji.

Kwa taarifa hizo ni wazi Kompany anaenda kuandaliwa kuwa kocha wa club ya Anderlecht,  Kompany anaondoka Man City akiwa kaichezea jumla ya michezo 360, akifunga magoli 20, mataji 4 ya EPL, League Cup 4, FA Cup 2 na Ngao ya Jamii 2. Kompany alianzia soka lake katika Academy ya Anderlecht akiwa na umri wa miaka 14 2000 na 2003 akapandishwa timu ya wakubwa ya Anderlecht na kucheza kwa misimu mitatu, 2006 akajiunga na club ya Humberger SV aliyodumu nayo kwa misimu miwili na kwenda Man City 2008.

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)….Soma Hapa Uwe Tajiri

Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.
 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 
Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.
Usafi wa vyombo na mazingira ya kukuUchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.
2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.
3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.

Magonjwa na kinga kwa kuku wote
1.Ndui ya kukuHuathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.
2.Mdondo/kideriMdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
3.Ukosefu wa vitamini AUgonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.
4.KosidiosisiHuathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.
5.Viroboto, chawa na utitiriHawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.
6.MinyooMinyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.

Chakula cha ziada1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.
2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).
3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.
4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.
5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.
6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.
Utotoleshaji wa vifarangaChagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.
Sifa za jogoo bora1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.
2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.
Sifa za tetea boraTetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.
Uhifadhi wa mayai1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.
3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.
4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
Kuatamiza mayai1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.
2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.
3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.
4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.
5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti
Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;
2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.
3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.
Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifoVifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;
Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.
Chanjo ya mdondo kideri/lufuoKama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3
Kinga dhidi ya kosidiosisiKinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.
1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.
2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba
3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;
Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu
Hitimisho1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.
2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja
3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.
5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.
7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.
8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.

Waziri Mwakyembe ampongeza Mbwana Samatta

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ametoa pongezi kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuibuka mabingwa wa Ubelgiji.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Samatta amefanya jambo kubwa kwa kuzingatia Ubelgiji ni moja ya mataifa makubwa tena yanayofanya vizuri kwenye mchezo wa soka duniani.

”Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo”, amesema.

Mbwana Samatta ambeye ni mchezaji wa zamani wa Simba, TP Mazembe na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016, mpaka sasa ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Ubelgiji akiwa amefunga magoli 20.

Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ambapo mwaka huo pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.

UFAHAMU UGONJWA WA NGIRI NA TIBA YAKE*

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.
Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).
Dalili za NgiriTumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.
Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521

Spika Ndugai Apigilia Msumari Sakata la Mbunge Stephen Masele Kuhojiwa Kamati Ya Maadili

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele, hawezi kukaidi tena agizo la kutakiwa kufika Kamati ya Maadili baada ya kuitwa na Spika huyo kwa mara ya pili. Akizungumza na waandishi wa habari Spika Ndugai amesema suala la Bunge kumuita Masele halihusiani na matukio yaliyotokea Afrika Kusini bali ni kwa sababu ya mambo aliyofanya nyumbani.
“Ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu wa nidhamu, anaunganisha hilo na matendo anayoyafanya huko, lakini hatujamuita kwa mambo ya South Afrika Watanzania watulie baada ya muda zitaletwa bungeni kila mtu atasikia kuhusu anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa nini na wataelewa kama ameonewa au hajaonewa.
“Stephen Masele hawezi kukaidi zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania, labda sababu awe mkimbizi na  akirudi Tanzania lazima aje Kamati ya Maadili, ni wito wa kisheria tunachomuitia ni tabia yake uchonganishi wa viongozi, kwa sasa hatuwezi kusema ila akishatoka mtaelewa fitina ikoje, ambayo ni kukosa sifa kwa kiongozi yeyote yule”, amesema Spika Ndugai.

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.
Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).
1. Sukari.Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.
2. Lehemu (Cholesterol).Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.
3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.
Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku – control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari. 

Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0759208637 au 0620510598

Sababu 5 Kwanini Wasanii Tanzania Hupenda Kuoa nje

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii wa Tanzania kuoa nje ya nchi yao, hali inayopelekea watu wengi kujiuliza kuna shida gani kwa wanawake wa Tanzania.

Wasanii kama Alikiba, Ben Pol na AY, wote wamefanikiwa kuoa nje ya nchi, huku Ben Pol akiwa mbioni kumuoa mpenzi wake Anerlisa ambaye ni raia wa Kenya baada ya kumvisha pete ya uchumba hivi karibuni. Alikiba pia ameoa Kenya na AY amemuoa mrembo raia wa Rwanda.

Mwijaku ambaye ni muigizaji maarufu nchini na mtu maarufu katika mitandao ya kijamii, amezitaja sababu 5 zinazopelekea wasanii wa Tanzania kuamua kuoa nje ya nchi.

Sababu ya kwanza ameitaja kuwa ni uoga wa wasanii wa kiume maarufu Tanzania, kutokana kuwa wanahisi wanawake wa Kitanzania wanawafahamu nje ndani.

Sababu ya pili ni kuogopa kuchaguliwa au kukosolewa uchaguzi wa wanawake wao na ndugu wa familia. Mtazame hapa chini Mwijaku akielezea zaidi sababu hizo.

”Nafuatwa na wanaume 500 kwa siku” – Miss Bella

KwaMsanii wa Bongo Fleva Isabela Mpanda ‘Miss Bella’ amesema kuwa hutongozwa na wanaume ambao idadi yao inaweza kufikia 500 kwa siku na haoni ajabu kwake kama mwanamke.

Bella amesema kuwa kufuatia hali hiyo ya kufuatwa sana limepelekea pia kuhongwa vitu vya gharama, lakini hategemei mali wala kitu chochote kutoka kwa mwanaume ili aendeshe maisha yake kama wanavyofanya baadhi ya mastaa wa kike badala yake anapambana kivyake kufikia malengo yake.

“Sishangai na sio ajabu mimi kuhongwa lakini sitegemei sana hivyo vitu vya kupewa mimi najipambania mwenyewe”, amesema Bella.

Bella amekuwa akiingia kwenye migogoro na baadhi ya watu kwenye mitandao, ambao wamekuwa wakidai kuwa anaigiza maisha ya kwenye mitandao na si maisha yake halisi.