De Oranje are ready to rise again.

Kila taifa lina muundo na utamaduni ambao unaleta ladha ya soka lake.:✍️Mwaka 1974 Uholanzi ilisheheni vipaji vikubwa sana. Licha ya kuwa na kizazi cha dhahabu wakashindwa kunyakua kombe la dunia. Kikosi kile kilitajwa kuwa kikosi bora sana katika historia ya soka.:✍️ 2010 walijitahidi kufikia kuweka historia ya kunyaku taji la lakini wakazidiwa na Wahispania. Uholanzi ile ilishehen kizazi cha dhahabu haswa. Akina Roben, Van De Sar, Welsej n.k.:✍️ Baada ya 2014, Uholanzi ikatoka kwenye Total Football na kwenda Total Failure. Pombe kali ikalevya kizazi cha waholanzi. Soka lao likawa butu.:✍️ Swahiba wangu mmoja anayeishi Uholanzi aliniambia akipokwenda Uholanzi mwaka 2012, asilimia kubwa ya waoto wa miaka 9+ utamkuta aidha anacheza vilabu vya mtaani au yupo kwenye akademi ya soka ya klabu kubwa.:✍️ Akaniambia miaka 8 ijayo uholanzi itaisha sana. Kila kijana hapa ana ndoto ya kuwa Cryjuff au Roben.:✍️ Mtaa kama Tandale unakuta una vilabu sio chini ya 7. Jambo la kuvutia utakuta Vipo vilabu vidogo kabisa vya watoto wa chini ya miaka 9.:✍️Madhara yake tumeona kizazi cha sasa vha Uholanzi. Tazama ile cream ya Ajax, angalia nyongo za Van Djik, Gigi zilivyochafukwa. Hata yule Depay aliyembwele OT nae amekuwa wa moto.:✍️ Ukitaka kuamini maneno yangu, leo watazame hawa vijana wakisakata kabumbu vs England:De Oranje are ready to rise again.

Mapacha Paul na Peter Okoye wa P-Square kuburuzana mahakamani kisa picha

Wasanii wakubwa nchini Nigeria, ambao pia ni mapacha Peter na Paul Okoye huenda wakaburuzana mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa Paul ametumia picha ya mwenzie kwenye tangazo la tamasha lake nchini Angola.

Peter ambaye yeye ndiye mlalamikaji, amesema kuwa anatarajia kwenda mahakamani kumshtaki ndugu yake, Paul Okoye, kwa kutumia picha zake kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo la muziki.

Kwahiyo wameamua kutumia picha yangu ili wauze tiketi za show yao huko Angola. Nyie mapromota na uongozi mzima mwanasheria wangu atalifuatilia suala hilo mapema iwezekanavyo,” ameandika Peter kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, tayari Paul Okoye ameshafanya show yake jana Jumapili Mei 26, 2019 usiku nchini Angola.

Peter na Paul ni mapacha na zamani waliunda kundi la P-Square ambalo lilipata umaarufu zaidi duniani kupitia nyimbo kadha wa kadha ikiwemo Personally, Temptation na nyinginezo.

Kwasasa kundi hilo limevunjika kwa sababu mbalimbali ikiwemo za maslahi binafasi na kifamilia, Ingawaje kumekuwa na masuluhisho kadhaa ya kurudisha kundi hilo.

Cardi B aahirisha tamasha lake kisa upasuaji

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Cardi B amejitoa kutumbuiza kwenye tamasha la 92Q Spring Bling Ijumaa hii mjini Maryland kutokana na kupata tatizo baada ya upasuaji wa kutengeneza mwili (liposuction) alioufanya baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na rapper huyo vimeeleza kuwa kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kupona baada ya kufanya pia upasuaji wa maziwa yake na madaktari wameshauri kuwa Cardi B anahitaji mapumziko ya muda mrefu ili mwili wake urudi kama zamani kutokana na baadhi ya sehemu alizofanyiwa upasuaji

Shamsa Ford ajitangaza kuwa single.

 Shamsa Ford na Mume wake ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini Chid Mapenzi penzi lao linasemekana  kuwa limevunjika, ingawa kwa upande wao hakuna aliyefunguka kuhusu hilo.

Tetesi hizo zimezidi kusambaa kwenye mtandao kijamii baada ya caption aliyoiandikaShamsa kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amejiita single mama na ndipo mashabiki walipopigia msitari na kusema kuwa ndoa kati ya Shamsa na Chid Mapenziimevunjika, ndoa hiyo ilifungwa September 2, 2016.

“Morning my people..kumekucha jamani ..wale masingle ladies kama mm jamani achieni mashuka mkatafute vijicent vya watoto wenu maana mjini pagumu bila kuchakarika na hizi shule za watoto wetu vingereza vingi mpaka mtu unaogopa kurudi nyumbani mapema unavizia mpaka mtoto awe amelala😀”

Real Madrid wamaliza La Liga kwa kipigo nyumbani kwao.

Zinedine Zidane amesema kuwa hatamtumia tena msimu ujao mshambuliaji wake, Gareth Bale .Zidane amesema kuwa kwenye mchezo huu wa mwisho asingeli muingiza Bale, hata kama wachezaji wote wa sub wangeisha.

“Sitamjumuisha (Bale) kwenye kikosi changu cha msimu ujao, kuhusu mchezo huu kumuaga kwa heshima sikufikiria. Nadhani hata wachezaji wa ziada wangeisha nisingeweza kumuingiza uwanjani,” amesema Zidane.Real Madrid wamemaliza msimu huu wakiwa nyuma ya alama 21 nyuma ya mabingwa wapya wa La Liga FC Barcelona.